Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Bokova afanya ziara nchini Burkina Faso,akutana Rais Compaore.

Bokova afanya ziara nchini Burkina Faso,akutana Rais Compaore.

Mkurugenzi mkuu wa Shirika la elimu , sayansi na utamaduni la Umoja wa Mataifa UNESCO Irina Bokova amethibitisha kujitolea kwa shirika hilo kwa mwaka wa kimataifa wa ushirikiano wa sekta ya maji ambao unaoongozwa na shirika hilo.

Bokova ameyasema hayo katika mazungumzo na Rais Blaise Compaore wa Burkina Faso nchini humo wakati wa ziara rasmi ambapo pia alitembelea taasisi kadha za kisayansi zinazohusika na masuala ya maji.

Viongozi hao walizungumzia pia hatua za UNESCO za kusaidia bara la Afrika wakigusia Mali ambako linasaidia kuhifadhi urithi wa kitamaduni

Akiwa nchini Burkina Faso, Bi. Bokova alikabidhiwa tuzo ya juu zaidi nchini humo  kwa kujitolea kwake katika kuliongoza Shirika la UNESCO na jitihada zake ya kuketa amani  barani Afrika hususan nchini Mali.