Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Uhuru na haki za binadamu ni muhimu kwa UM: Ban

Uhuru na haki za binadamu ni muhimu kwa UM: Ban

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki- Moon amesema uhuru na haki za binadamu ni mambo muhimu ambayo yanasaidia kusongesha mbele shughuli za Umoja huo.

Katika ujumbe wake aliotoa kwa njia ya video kwenye mkutano wa Baraza la Haki za Binadamu mjini Geneva, Uswisi, Bwana Ban amesema baada ya kuanzishwa kwa Umoja wa Mataifa, mwaka 1945, nchi wanachama ziliunda Baraza hilo ambalo lina wajibu wa kulinda misingi ya chata iliyoanzisha Umoja wa Mataifa na tamko la kimataifa la haki za binadamu.

Amesema miongo miwili baadye azimio la aina yake la Vienna na mpango kazi vilipitishwa ili kuimarisha jitihada za utetezi wa haki za binadamu.

(SAUTI YA BAN)