Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

ITU yazungumzia elimu kwa njia ya mtandao

ITU yazungumzia elimu kwa njia ya mtandao

Shirika la kimataifa la mawasiliano, ITU limesema kuwa mitandao ya intaneti yenye kasi kubwa zaidi yaweza kuimarisha mfumo wa elimu duniani na kusaidia kufikia lengo la maendeleo la milenia la elimu kwa wote. Taarifa ya ITU imekariri ripoti mpya ya tume ya maendeleo ya mitandao ya kasi na mfumo wa digitali inayoeleza kuwa mitandao hiyo inaweza kutoa fursa ya kuwepo kwa programu za elimu mtandao na hivyo kuwezesha wanafunzi wenye uwezo wa juu kitaaluma katika nchi maskini kusaidia nchi zao kuondokana na umaskini.  Mathalani ripoti hiyo imesema wanafunzi wanaoelimika kupitia elimu mtandao inayoweza kutekelezwa kwa kutumia simu za mikononi na hata kompyuta wanaweza kuwa watafiti, watunga sera na hata wajasiriamali.