Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Mikakati yaanza kudhibiti wahamiaji haramu: IOM

Mikakati yaanza kudhibiti wahamiaji haramu: IOM

Shirika la kimataifa la kuhudumia wahamiaji IOM, linakutana nchini Tanzania na maafisa uhamiaji kutoka Msumbiji, Malawi na wenyeji wa Tanzania kwa lengo la kubainisha mbinu za kisasa za kukabiliana na wimbi la wahamihaji haramu. Mkutano huo wa siku tatu, unafanyika wakati ambapo kiwango cha wahamiaji haramu kutoka eneo la Pembe ya Afrika wanaomiminika nchini Tanzania na maeneo ya nchi nyingine jirani kikiripotiwa kuongezeka na kutishia ustawi wa eneo hilo. Taarifa zaidi na George Njogopa.

(SAUTI GEORGE)