Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Hospitali ya kutembea yaleta nafuu Somalia

Hospitali ya kutembea yaleta nafuu Somalia

Wakazi wa maeneo kadhaaa ya Somalia wananufaika na huduma ya hospitali inayotembea ambayo imeanzishwa  ikiwalenga wakimbizi waliolazimika kuhama makazi yao kutokana na  ukame na mapiganao yanayofanywa  na kundi la kigaidi la Al- Shabaab.  Hospitali hiyo inayohudumia takribani watu elfu tatu katika kambi ya KARIBU, na ambayo inamilikiwa na Jeshi la Somali na kudhaminiwa na Ujumbe wa Umoja wa Afrika nchini humo, imekuwa msaada mkubwa, kama anavyoeleza Mwenyekiti wa kambi  hiyo Isack Hassan Abdi,

(SAUTI YA HASSAN ABDI)

 Huduma za hospitali zinazotembea nchini Somalia zinatajwa kama msaada mkubwa kwa wanachi waliosambaa maeneo mbalimbali kutokana na mapigano. Hamdi Abdulla, ambaye ni mmoja wa wauguzi anasema wengi wa wagonjwa wanaofika kutibiwa wana magonjwa yanayosababishwa na utapiamlo na lishe mbovu.

(SAUTI YA HAMDI ABDULLA)