Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Njia mpya yapatikana kufika Mali Kaskazini: WFP

Njia mpya yapatikana kufika Mali Kaskazini: WFP

Shirika la mpango wa chakula duniani, WFP, limeanzisha njia mpya kwa ajili ya kufanikisha safari za ardhini kuwasambaza huduma muhimu kwa maeneo yanahohitaji misaada ya dharura kaskazini mwa Mali.

Hivi sasa misaada ya muhimu inasafirishwa kupitia njia inayoanzia mji mkuu wa Niger Niamey na kulekea moja kwa moja hadi kaskazini mwa Mali ambako kunashudia hali ya ukosefu wa chakula na mahitaji mengine muhimu.

Tayari magari makubwa yameshafikisha kiasi cha tani 200 za chakuka katika mji wa Menaka na misafara mingine zaidi inaelekea huko. George Njogopa na taarifa zaidi

(SAUTI YA GEORGE)