Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Hali ya watu milioni 1.2 kaskazini mwa Mali inatia wasiwasi: OCHA

Hali ya watu milioni 1.2 kaskazini mwa Mali inatia wasiwasi: OCHA

Shirika la kuratibu masuala ya kibinadamu la Umoja wa Mataifa OCHA limeelezea wasi wasi wake kuhusiana na hatma ya watu zaidi ya milioni 1.2 kaskazini mwa Mali ambao wameathiriwa na oparesheni za kijeshi. Hata hivyo kumekuwa na dalili za kuyafikia maeneo ya kati mwa Mali na pia kwa kiwango cha kidogo maeneo ya Kaskazini kufuatia kufunguliwa kwa barabara inaoyunganisha kati kati na kaskazini mwa Mali. Hali inasalia kuwa tete huku makadirio ya hivi majuzi yakionyesha kuwa watu 16,000 wamelazimika kuhama makwao ndani mwa Mali huku maelfu ya wengine wakivuka mipaka na kuingia nchi majirani zikiwemo Mauritania, Burkina Faso na Niger tangu mwazo wa mwaka huu. Jens Laerke ni msemaji wa OCHA

(SAUTI YA ANDREJ MAHECIC)

Mkurugenzi wa oparesheni za OCHA John Ging kwa sasa yuko nchini Mali kujionea hali ilivyo baada ya mapigano ya hivi majuzi na hali ya huduma za kibinadamu.

Wakati huo huo Shirika la kuhudumia watoto UNICEF limesema kuwa machafuko yaliyolikumba eneo la kaskazini mwa Mali, yamasababisha kuvuruga shughuli za elimu kwa zaidi ya watoto 700,000 huku wengine kiasi cha 200,000 wameendelea kukwama kwenye maeneo yenye machafuko.