Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Mongolia yatajwa kuwa mwandalizi wa siku ya mazingira mwaka huu

Mongolia yatajwa kuwa mwandalizi wa siku ya mazingira mwaka huu

Taifa la Mongolia ambalo limelipa kipaumbele suala la uchumi usioathiri mazingira kwenye sekta zake za kiuchumi zikiwemo sekta za uchimbaji madini na kutoa hamasisho kwa vijana litakuwa mwandalizi wa siku ya mazingira duniani mwaka huu siku ambayo itadhimishwa tarehe tano mwezi Juni.  Kauli mbiu ya siku hiyo inajulikana kama Think.Eat.Save. Reduce Your Foodprint ikiwa inaipa msukumo kampeni ya kimataifa ya kuzuia utupaji wa chakula iliyozinduliwa mapema mwaka huu na Shirika la mazingira la Umoja wa Mataifa UNEP, Shirika la  kilimo na mazao la Umoja wa Mataifa FAO na washirika wao.  Tangazo hilo lilitolewa wakati wa kukamilika kwa kikao cha baraza kuu la UNEP kilichohudhuriwa na mamia ya mawaziri wa mazingira, maafisa wakuu kutoka Umoja wa Mataifa na waakilishi wa mashirika ya umma ambao walikusanytika kujadili masuala ya mazingira likiwemo suala ya utupaji wa chakula. Mongolia ndilo taifa linalokua kwa hara zaidi duniani.