Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

UM wawasihi wakazi wa Jonglei kuacha mapigano

UM wawasihi wakazi wa Jonglei kuacha mapigano

Mkuu wa ofisi ya Umoja  wa Mataifa nchini Sudan Kusini Hilde Johnson, amehitimisha ziara yake ya siku mbili kwenye jimbo la Jonglei nchini humo na kutaka jamii ziache mwendelezo wao wa ghasia. Ziara hiyo ilifanyika baada ya tukio la hivi karibuni la wizi wa mifugo na mashambulizi kwa dhidi ya raia kwenye jimbo hilo ambapo makumi kadhaa ya raia waliuawa.  Bi. Johnson alisema mashambulizi hayo yalikuwa makubwa na kutishia utulivu wa jimbo la Jonglei ambapo katika mazungumzo na Gavana wa jimbo hilo Kuol Manyang Juuk alitoa pia rambi rambi zake kwa wafiwa.

(SAUTI YA HILDE)

"Natoa rambirambi zangu kwa kweli tunapenda kuona utulivu katika jimbo la Jonglei. Na jambo la msingi kabisa ni kufahamu ofisi yetu inaweza kufanya kitu gani kwenye mazingira ya sasa ili mwendelezo huu wa ghasia unakomeshwa na kwamba tunazuia ghasia hizo kusababisha mauaji zaidi.”