Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Ban akutana na waziri wa mambo ya nje wa Ugiriki

Ban akutana na waziri wa mambo ya nje wa Ugiriki

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Kin Mon amefanya mazungumzo na Waziri wa mambo ya nje wa Ugiriki Dimitris Avramopoulos ambapo wamejadili hali ya kisiasa Mashariki mwa Mediteranian, na pia kuangazia matarajio ya kuanza tena mazungumzo ya kutafuta suluhu la kina huko Cyprus, pamoja na kutafuta suluhu kwa mgogoro kuhusu jina kati ya Ugiriki na Jamhuri ya zamani ya Kiyugoslavia ya Macedonia.

Bwana Ban amesisitiza umuhimu wa kuongeza kasi katika harakati za kutafuta suluhu kwa mizozo yote hiyo miwili, na kuelezea kujitolea kwake binafsi kuona hilo linatimia.