Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

UM watoa tahadhari ya baa la njaa kufuatia mafuriko Musumbiji

UM watoa tahadhari ya baa la njaa kufuatia mafuriko Musumbiji

Taarifa ya timu ya Umoja wa mataifa nchini Msumbiji inaonyesha  Kwamba huenda mvua kubwa ikaendelea kunyesha na kusababaisha mafuriko makali zaidi katika ukanda wa kati na kaskazini mwa Msumbiji.  Taarifa hii inakuja wakati huu ambapo kumekuwa na mlipuko wa kipindupindu katika jimbo la Cabo Delgado lililoko Kaskazini mwa Msumbiji ambapo watu 413 wameripotiwa kuugua huku wawili wakifariki dunia.  Kadhalika Uchunguzi wa awali unaonyesha kwamba zaidi ya watu laki moja na tisini na moja elfu wameathiriwa na mafuriko huku pia mashamba ya zaidi ya watu laki moja na elfu sitini na sita yakiwa yameharibiwa vibaya.  Taarifa hiyo ya timu ya Umoja wa Mataifa nchini Msumbiji imetahadharisha kuchukuliwa kwa hatua za dharura ili kuinusuru nchi hiyo na baa la njaa kwa kupendekeza msaada wa mbegu.