Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

WFP yaonya juu ya tatizo la chakula Yemen

WFP yaonya juu ya tatizo la chakula Yemen

Shirika la mpango wa chakula duniani WFP limeonya juu ya kitisho cha ukosefu wa chakula inayoikabili Yemen ikisema kuwa hali ya ukosefu wa chakula huenda ikapindukia kuzidi ile ya mwaka uliopita 2012.

WFP imesema kuwa, hali ya uzalishaji chakula imeporomoka kiasi cha kuzua kitisho ambacho kinaweza kuzorotesha ustawi wa kijamii.

Imesema kuna wasiwasi wa familia nyingi ikiwemo zile za mijini na maeneo ya vijijini zikashindwa kumuda gharama za chakula kutoka gharama yake kuwa juu.

Yemen imekuwa ikukumbwa na mzozo wa kisiasa hali iliyosababisha baadhi ya maeneo kutoendelea na shughuli za uzalishaji mali.