Makubaliano ya Doha kuhusu Darfur yapewa msukumo
Mkutano uliozileta pamoja ujumbe wa pamoja wa Afrika na Umoja wa Maitafa huko Darfur, UNAMID na ofisi ya Umoja wa Mataifa huko Sudan, UNCT umejadili kwa kina njia bora ya kuupa msukumo mpango wa amani katika jimbo la Darfu uliosaniwa Doha, baina ya serikali na kundi la waasi . Mkutano huo umeangazia njia zinazoweza kusaidia kuyapa uhai zaidi makubaliano hayo ambayo kimsingi yanafungua njia ya kumaliza vita katika jimbi hilo. Mkutano huo uliofanyika kwenye makao makuu ya UNAID El Fasher, Kaskazini mwa Darfur ulihudhiriwa pia na maafisa shirika la maendeleo ya Umoja wa Mataifa UNDP na ofisi ya uratibu na majanga ya kibinadamu Taarifa zaidi na George Njogopa.
(SAUTI YA GEORGE)