ILO yasaidia harakati za uhifadhi wa mazingira Kenya

21 Februari 2013

Shirika la kazi duniani, ILO nchini Kenya na taasisi ya kuwezesha wanawake nchini humo, Kenya Women Finance Trust wameibuka na mradi wa kusaidia kuhifadhi mazingira na wakati huo huo kuinua kipato cha wanawake.

Mradi huo wa miaka miwili utakaoanza mwezi Aprili mwaka huu unalenga kuwapatia mikopo wanawake vijana ili waweze kununua taa aina ya kandili zinazotumia nishati ya jua na kuziuza kwa wanawake hususan wa vijijini wasio na umeme ili waache kutumia taa za mafuta ya taa ambazo siyo tu zinaharibu mazingira bali pia moshi wake unaathiri afya zao.

ILO inasema kuwa matumizi ya taa hizo za kandili za nishati ya jua zinagharimu karibu dola Sitini lakini faida yake ni kubwa kuliko matumizi ya taa zinazotumia mafuta ya taa.

George Waigi ni Mratibu wa kitaifa wa mradi wa ILO wa kuwawezesha vijana wajasiriamali.

(SAUTI YA WAIGI)

Kwa mujibu wa shirika la mazingira duniani, WFP, gharama za kutumia nishati ya jua zinaweza kurejeshwa ndani ya kipindi cha mwaka mmoja.

 

♦ Kupata takwimu za waathirika vitani Ukraine bofya  hapa.
♦ Iwapo ungependa kupokea taarifa kutoka UN News Kiswahili kila wakati zinapochapishwa jisajili  hapa.
♦ Pia unaweza kupakua apu ili kusikiliza matangazo yetu wakati wowote popote ulipo.
♦ Tembelea pia chaneli yetu ya Youtube na pia Soundcloud na Twitter