Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Harakati za maendeleo Burundi zazidi kupatiwa shime

Harakati za maendeleo Burundi zazidi kupatiwa shime

Msaidizi wa Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa ambaye pia kiongozi mshirika wa shirika la Maendeleo la Umoja huo UNDP Rebecca Grynspan ameanza ziara  ya siku tatu nchini Burundi inayonuwia kuweka mikakati ya kuistaawisha  nchi hiyo kimaendeleo baada ya kukumbwa na vita vya wenyewe kwa wenyewe. Bi Grynspan mbali na kukutana na viongozi mbalimbali  wa Burundi atapata fursa ya kushuhudia binafasi miradi inayodhaminiwa na Shirika hilo. Kutoka Bujumbura, Muandishi wetu Ramadhani KIBUGA anatuarifu zaidi.

(SAUTI YA Ramadhani)