Maandalizi ni muhimu kabla ya kupeleka vikosi vya kulinda amani: Ladsous

20 Februari 2013

Umoja wa Mataifa umetakiwa kujenga kile kinachoitwa maandalizi ya awali wakati wa kuelekea kwenye operesheni za amani katika nchi za Mali, Syria na eneo la Pembe ya Afrika.

Mkuu wa masuala ya ulinzi wa amani ndani ya Umoja wa Mataiaf Hervé Ladsous, amesema hayo wakati akizungumza na kamati maalumu inayohusika na ulinzi wa amani inayofahamika kama C34.

Akitolea mfano hali mbaya ya kisiasa na usalama inayoliandama eneo la Sahel, mwanadiplomasia huyo amesema kuwa Umoja wa Mataifa unapaswa kutambua mapema changamoto kubwa iliyo mbele wakati huu ambapo kuna uwezeano mkubwa wa kupeleka vikosi vyake vya uangalizi wa amani huko Mali, Somalia na Syria.

Bwana Ladsous amesema mgogoro mkubwa wa kisiasa, kiusalama na kibinadamu huko ukanda wa Sahel unaweka bayana kabisa uwezekano wa kupelekwa kwa kikosi cha ulinzi wa amani cha  Umoja wa Mataifa kwenye eneo hilo.

 

♦ Kupata takwimu za waathirika vitani Ukraine bofya  hapa.
♦ Iwapo ungependa kupokea taarifa kutoka UN News Kiswahili kila wakati zinapochapishwa jisajili  hapa.
♦ Pia unaweza kupakua apu ili kusikiliza matangazo yetu wakati wowote popote ulipo.
♦ Tembelea pia chaneli yetu ya Youtube na pia Soundcloud na Twitter