Skip to main content

Ban azungumzia ukosefu wa haki ina usawa duniani

Ban azungumzia ukosefu wa haki ina usawa duniani

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-Moon amesema kutokuwepo kwa usawa na haki miongoni mwa jamii kunazorotesha juhudi za jumuiya za kimataifa katika kuwakwamua mamilioni ya raia katika umaskini. Taarifa zaidi na Alice Kariuki.

(SAUTI YA ALICE KARIUKI)

Taarifa zaidi na ALICE KARIUKI …………

Katika ujumbe wake wa kuadhimisha siku hiyo ya kimataiaf ya haki na usawa duniani hii leo Bwana Ban amesema inasikitisha kuona fursa nyingi haziwafikii waliowengi huku pia kukosekana kwa usawa kukiongezeka.

Amesema hali hiyo inachangia kipato kidogo kwa idadi kubwa ya wanawake na vijana jambo linalosababisha kukosekana kwa huduma za uhakika za elimu afya na ajira.

Katibu Mkuu huyo wa umoja wa mataifa ametaka kuimarishwa na kujengwa kwa taasisi na sera shirikishi ili kuleta maendeleo.

Akizungumzia utekelezaji wa Malengo ya maendeleo ya milennia kama sehemu ya kukuza ustawi wa jamii,Bwana BAN amepongeza juhudi zilizofanywa na viongozi kote duniani katika kukuza fursa za ajira na kuimarisha huduma za kijamii kama sehemu ya ahadi zilizotolewa na viongozi hao.

Amesema uwazi na majadiliano yenye lengo la kuleta mandeleo endelevu na usawa ni muhimu katika juhudi za kukuza jamii yenye haki na usawa.