Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Si sahihi mahakama ya kijeshi kutumika kuhukumu raia: Pillay

Si sahihi mahakama ya kijeshi kutumika kuhukumu raia: Pillay

Ofisi ya Umoja wa Mataifa juu ya haki za binadamu imesema imesikitishwa na kitendo cha Sahara Magharibi kutumia mahakama za kijeshi kuendesha kesi zinazowahusu raia ikisema kuwa hatua hiyo uvunjifu wa haki za binadamu.

Mamlaka katika eneo la Sahara Magharibi imeripotiwa, kuwatia hatiani raia 25 kwa kutumia mahakama za kijeshi. Mahakama hiyo ya kijeshi ambayo ni tiifu wa mamlaka ya Rabat imetoa adhabu ya kifungo cha miaka kati ya miwili hadi maisha kwa watu waliokutikana na hatia wakati kulipozuka wimbi la maandamano miaka mitatu iliyopita. Wakati wa maandamano askari jeshi kadhaa wanadaiwa kupoteza maisha