Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Ripoti ya UM yaweka bayana athari za mazingira kwa mfumo wa endokrini

Ripoti ya UM yaweka bayana athari za mazingira kwa mfumo wa endokrini

Ripoti ya shirika la Umoja wa Mataifa linalohusika na mazingira UNEP imesema kuwa matumizi ya kemikali ambazo hazifanyiwa uchunguzi  zinaweza kuleta hitalafu katika mwili wa binadamu ikiwemo kuvuruga mfumo wa homoni. Ripoti hiyo ambayo pia imeandaliwa kwa pamoja pia na shirika la afya ulimwenguni WHO imekariri mfumo wa kisanyansi unaojulikana Endokrine ambayo ni mahsusi kwa ajili ya kuwezesha mwili kutoa vichocheo vinavyoingia katika mzunguko wa damu imeeleza kuwa hali hiyo inakutikana zaidi katika maeneo yenye uzalishaji mkubwa viwandani.  Imesema hata hivyo hali hiyo inaweza kupunguzwa na kuwa katika kiwango cha kuridhisha iwapo kutafanyika kile kiluchokiita upiamaji na uchunguzi wa mara kwa mara. Taarifa zaidi na George Njogopa:

(Taarifa ya George)