Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Mkutano wa kimataifa kuhusu mazingira na chakula waendelea Nairobi

Mkutano wa kimataifa kuhusu mazingira na chakula waendelea Nairobi

Suala la utupaji wa chakula ni moja ya ajenda kuu zinazozungumziwa mwenye mkutano wa kimataifa unaowaleta pamoja mawaziri wa mazingira kutoka pembe zote za ulimwengu ambao kwa sasa umeingia siku yake ya pili mjini Nairobi nchi Kenya.

Inakadiriwa kuwa kiasi cha tani Bilioni 1.3 za chakula hutupwa kila mwaka duniani ambapo asilimia kubwa hupotea wakati kinapozalishwa hususan kwenye nchi zinazoendelea kinyume na kwenye nchi zilizostawi ambapo chakula hutupwa wakati wa kuliwa.

Tristran Stuart ni ni mwandishi wa vitabu na mwanahistoria raia wa Uingereza ambaye pia ni mwanzilishi wa Shirika la “Feeding the 5000” linalotoa hamasisho kuhusu umuhimu na njia za kuzuia kutupwa kwa chakula na ni mmoja wa wanaohudhuria mkutano huo.

(SAUTI YA TRISTRAN)

Mkutano huu umendaliwa na Shirika la mazingira la Umoja wa Mataifa, UNEP na unajadili masuala yanahusiana na mazingira yakiwemo utunzi wa misitu , athari za kemikali kwa afya ya binadamu na mzingira ikiwemo mabadiliko ya hali ya hewa.