Japan kutekeleza mfumo wa breki za gari wa kuzuia ajali barabarani

19 Februari 2013

Taifa la Japan mwezi huu litaanza kutekeleza hatua ya kuhakikisha usalama kwenye malori na mabasi kuambatana na kanuni nambari 13 ya tume ya uchumi ya Umoja wa Mataifa barani Ulaya UNECE kuhusu mfumo maalum wa breki za magari ikiwa ndiyo nchi ya 43 kutekeleza kanuni hiyo.

Tume hiyo inasema kuwa kuanza kutumika kwa kanuni hiyo kutafanya kutumika kwa mfumo huo wa breki kwa gari kuwa wa lazima kwa malori na mabasi yote mapya yanayoundwa nchini Japan.

Mfumo huo unaboresha usalama wa gari kwa kutambua mapema kasoro wakati gari linapoendeshwa ambapo breki huagizwa kulisimamisha gari moja kwa moja na kulielekeza linakostahili kuenda. Mfumo huu ambo umekuwa ukitumiwa barani Ulaya awali  pia hulifanya gari kutopingira.

Kulingana na idara ya polisi nchini Japan, kuanzia mwezi Januari hadi mwezi Disemba mwaka uliopita zaidi ya ajali mbaya 400 ziliripotiwa hasa kwenye sehemu ambazo vifaa hivyo vinastahili kutumika