Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Hali yausalama bado kikwazo katika usambazaji misaada Syria:WFP

Hali yausalama bado kikwazo katika usambazaji misaada Syria:WFP

Shirika la mpango wa chakula la Umoja wa Mataifa, WFP limesema licha ya kwamba limeshiriki kwenye operesheni ya pamoja ya mashirika Umoja huo ya kusambaza misaada kwa wakimbizi walioko kambi ya Karameh nchini Syria, bado hali ya usalama si nzuri.

WFP imesema operesheni hiyo ya tarehe 16 mwezi huu katika mkoa wa Idleb kaskazini Magharibi mwa Syria iliwezesha mgao wa tani za ujazo 34 za vyakula kwa ajili ya watu Elfu Tano kwa kipindi cha mwezi mmoja.

Wafanyakazi wa WFP wamesema licha ya mgao huo bado hali ya chakula si nzuri ambapo baadhi ya wakimbizi wa ndani wanalazimika kuacha mlo mmoja ili waweze kuwapatia wenzao hivyo msaada wahitajika huku hali ya usalama ikiwa si nzuri.

Elizabeth Byrs ni msemaji wa WFP.

(SAUTI YA Byrs)