Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Ulimwengu waungana kupinga dhuluma dhidi ya wanawake katika kampeni ya “One Billion Rising”

Ulimwengu waungana kupinga dhuluma dhidi ya wanawake katika kampeni ya “One Billion Rising”

Kote duniani, watu wa tabaka mbalimbali walicheza muziki mnamo siku ya Alhamis, Februari kumi na nne, ambayo ni maarufu kama siku ya wapendanao,

Wengi wao walikuwa wakijiunga kwenye kampeni ya kimataifa ijulikanayo kama “One Billion Rising”, ya kupinga dhuluma dhidi ya wanawake.

Kauli mbiu ya kampeni hiyo katika Umoja wa Mataifa ilikuwa “Kataa ukatili wa majumbani, kataa ubakaji na uhalifu wa kingono.” Bi Michelle Bachelet ni Mkuu wa kitengo cha wanawake katika Umoja wa Mataifa, yaani UN Women, na huu ndio ulokuwa ujumbe wake:

Kampeni hiyo iliyoratibiwa na shirika lisilo la kiserikali la V-DAY, ilihusisha  kucheza muziki kwa pamoja kote duniani kwa lengo la kupaza sauti dhidi ya vitendo dhalili vinavyokandamiza haki za kibinadamu za wanawake na watoto wa kike.

Nchini Burundi, mwandishi wetu Ramadhan Kibuga alihudhuria hafla ya Kampeni hiyo, iloandaliwa na kituo cha Seruka ambacho hupokea wanawake waathirika wa vitendo vya ukatili, huku watu mitaani nchini Kenya wakizungumza na Jason kuhusu dhuluma dhidi ya wanawake.

Kampeni ya One Billion Rising, ambayo imeungwa mkono na kampeni ya Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa ya kupinga dhuluma dhidi ya wanawake iitwayo UNiTE, inafanyika siku chache kabla ya mkutano wa kila mwaka wa Tume ya Umoja wa Mataifa kuhusu hali ya wanawake, ambao utaanza tarehe 4 Machi. Mwaka huu, mkutano huo utaangazia kutokomeza na kuzuia aina zote za ukatili dhidi ya wanawake. Sikiliza makala yetu maalum kuhusu siku hiyo.