Kituo cha Seruka huko Burundi chapaza sauti kulinda haki za wanawake na watoto

16 Februari 2013

Utekelezaji wa vitendo dhalili dhidi ya wanawake na watoto wa kike unaendelea kupigiwa kelele kila uchwao na kwa kutumia mbinu mbali mbali kwa kuwa jamii zinazotekeleza vitendo hivyo nazo huibuka na mbinu mpya kila wakati ili kuweza kuendelea kukiuka haki za binadamu za wanawake na watoto wa kike. Nchini Burundi, ambako nako kuna vitendo vya ukatili dhidi ya wanawake ikiwemo vipigo na ubakaji, kituo cha Seruka cha mjini Bujumbura kiliandaa shughuli maalum kikitumia nyimbo na michezo ya kuagiza ili kuonyesha hali halisi ya ukiukwaji hiyo kwa lengo la kupaza sauti kwa niaba ya wale wasio na uwezo wa kusikika. Mwandishi wetu wa Maziwa Makuu Ramadhani KIBUGA alikuwa shuhuda wetu na ametuma ripoti hii.

 

♦ Kurambaza ukurasa mahsusi wa Siku ya Kiswahili Duniani bofya  hapa.
♦ Iwapo ungependa kupokea taarifa kutoka UN News Kiswahili kila wakati zinapochapishwa jisajili  hapa.
♦ Pia unaweza kupakua apu ili kusikiliza matangazo yetu wakati wowote popote ulipo.
♦ Tembelea pia chaneli yetu ya Youtube na pia Soundcloud na Twitter