Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

UM watuma wataalam wa haki za binadamu nchini Mali.

UM watuma wataalam wa haki za binadamu nchini Mali.

Huku hali ya usalama nchini Mali ikibaki kuwa tete, Ofisi ya Kamishina Mkuu wa Haki za Binadamu katika Umoja wa Mataifa imesema inawatuma wataalamu wa haki za binadamu kuchunguza hali ilivyo nchini humo.

Wataalamu watatu ambao tayari wamewasili mjini Bamako watachunguza madai ya ukiukaji wa haki za binadamu, yakiwemo madai ya ulipizaji kisasi. Cécile Pouilly kutoka afisi ya Kamishna wa Haki za Binadamu anaeleza zaidi kuhusu hatua ya kuwapeleka wataalam hao Mali.

(SAUTI YA Cécile Pouilly)