UM, Mashirika ya kiraia yaonya kuhusu baa la njaa CAR

15 Februari 2013

Tathmini iliyofanywa na Umoja wa Mataifa na mashirika yasiyo ya kiserikali kuhusu usalama wa chakula katika Jamhuri ya Afrika ya Kati (CAR), imeonyesha kuwa mizozo ya kisiasa na kijeshi kati ya mwezi Disemba mwaka 2012 na mwezi Januari mwaka huu, huenda ikatumbukiza nchi hiyo kwenye baa la ukosefu wa chakula. Maeneo mengi yaliyoshikiliwa na muungano wa waasi wa Seleka yanakabiliwa na hali ngumu kutokana na kusimama  kwa shughuli za kibiashara kwa kipindi kirefu. Kuna ripoti pia kuwepo kwa ongezeko la gharama za chakula zilizopanda kwa wastani wa asilimia 40. Baadhi ya kata zilizopo kwenye maeneo yanayodhibitiwa na kundi la Seleka zinakumbwa na uhaba wa chakula kutokana na mfumko wa bei. Joshua Mmali na taarifa kamili

(TAARIFA YA JOSHUA)