Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

IOM yasambaza misaada kwa waathirika wa mafuriko Chad

IOM yasambaza misaada kwa waathirika wa mafuriko Chad

Shirika la Umoja wa Mataifa linalohusika na uhamiaji IOM, limeanzisha juhudi za kusambaza misaada ya dharura kwa mamia ya watu waliokumbwa na mafuriko katika mji mkuu wa Chad N’Djamena na maeneo mengine ya jirani na kusababisha kiasi cha watu 98,000 kupoteza makazi yao na wengine 560,000 kuwa katika hali ya shida na taabu.

IOM kwa kushirikiana na maafisa wa serikali inasambaza huduma muhimu katika maeneo ya  Bongor, Hadjer Lamis  na N’Djamena yaliyoathiriwa zaidi na mafuriko hayo.

Mataifa kadhaa ya Magharibi ikiwemo Ujerumani imeanza kuchangisha mafunga ya fedha kwa ajili ya kufanikisha shughuli za usambazaji wa huduma za usamaria mwema ikiwemo mahitaji ya chakula na mengine ya kawaida.

Shirika la Mpango wa chakula duniani WFP limepeleka msaada wa chakula kuzikirimu zaidi ya familia 15,000 ambazo zipo kwenye mkwamo.