Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Tuwekeze katika ukusanyaji wa takwimu za afya: WHO

Tuwekeze katika ukusanyaji wa takwimu za afya: WHO

Viongozi wa takwimu za masuala ya afya waliokutana mjini Geneva, Uswisi kujadili ushirikiano wa siku za usoni katika kuboresha mbinu za makadirio ya takwimu kuhusu masuala ya afya wamehitimisha mkutano kwa kukubaliana  uwekezaji zaidi katika sekta hiyo. Mkutano huo uliandaliwa na shirika la afya duniani, WHO ambapo mathalani washiriki wamesema zaidi ya nchi 100 hazina mfumo wa kusajili vizazi na vifo na kwamba ni asilimia 34 ya nchi zote duniani zenye mfumo wa kisasa.

Dkt. Ties Boerma kutoka WHO amesema ukosefu wa takwimu sahihi kuhusu vizazi na vifo una athari katika maendeleo na kwamba takwimu sahihi ni muhimu katika kuelewa hali halisi ya sekta ya afya hivyo ni vyema kuwekeza zaidi.