Hafla ya madhehebu ya dini kuungana kwa ajili ya amani yafanyika kwenye UM

14 Februari 2013

Hafla maalum imefanyika leo kwenye makao makuu ya UM mjini New York, kuadhimisha kuanza kwa wiki moja ya Ushirikiano wa dini mbalimbali duniani, kama ilivyotangazwa na Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa katika azimio namba 65/5.

Hafla hiyo yenye kauli mbiu, “Kuungana kwa ajili ya desturi ya amani kupitia ushirikiano wa dini” imeandaliwa na afisi ya Rais wa Baraza Kuu na Shirika la Elimu, Sayansi na Utamaduni, UNESCO, pamoja na Kamati kuhusu Mashirika ya Kidini kwenye Umoja wa Mataifa.

Akiongea kwenye hafla hiyo, Rais wa Baraza Kuu, Vuk Jeremic amesema kila mmoja anatakiwa kurejelea mafunzo ya dini yake, kuheshimiana, kuonyesha huruma kwa walio wanyonge, na kutambua maumbile ya Mungu katika kila tu

(SAUTI YA VUK)