Makao Makuu ya UNPOS sasa kuhamia Mogadishu ili kuimarisha usaidizi wake

14 Februari 2013

 

Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa limepokea na kuridhia ripoti ya Katibu Mkuu  Ban Ki-Moon kuhusu hali ilivyo nchini Somalia ambayo pamoja na mambo mengine imependekeza kuhamisha ofisi ya Umoja huo kuhusu Somalia, UNPOS kutoka Nairobi, Kenya kwenda Mogadishu.

Ripoti hiyo iliwasilishwa na Tayé-Brook Zerihoun ambaye alisema kuwa hatua hiyo ni muhimu kwa kuwa wakati huu wa mabadiliko, fursa na changamoto zinazokabili Somalia zinahitaji ushiriki wa dhati wa Umoja wa Mataifa.

Hivyo amesema Katibu Mkuu Ban ametaka umoja wa Mataifa kujipanga upya kwa kuzingatia ripoti ya tathmini iliyofanyika mwaka jana iliyopendekeza Somalia kushika hatamu za mabadiliko kwa ushirikiano wa karibu zaidi na Umoja huo.

(SAUTI YA ZERIHOUN)

Bwana Zerhoun amesema kwa mujibu wa mapendekezo hayo ofisi za Umoja wa Mataifa zitakuwa zinahama taratibu kutoka Nairobi Kenya, kwenda Somalia katika kipindi cha miezi Sita hadi 12 ijayo.

 

 

♦ Kupata takwimu za waathirika vitani Ukraine bofya  hapa.
♦ Iwapo ungependa kupokea taarifa kutoka UN News Kiswahili kila wakati zinapochapishwa jisajili  hapa.
♦ Pia unaweza kupakua apu ili kusikiliza matangazo yetu wakati wowote popote ulipo.
♦ Tembelea pia chaneli yetu ya Youtube na pia Soundcloud na Twitter