Watu waendelea kulazimika kuhama licha ya waasi wa FARC Colombia kusitisha mapigano: OCHA

14 Februari 2013

Ofisi ya kuratibu masuala ya kibinadamu katika Umoja wa Mataifa, OCHA, imesema kuwa licha ya idadi ya mashambulizi kupungua, idadi ya watu wanaolazimika kuahama makwao nchini Colombia bado inaendelea kupanda kwa sababu makundi yenye silaha bado yanafanya mashambulizi.

Mashambulizi ya kundi lenye silaha la FARC yalishuka kwa asilimia 73 katika kipindi cha miezi miwili ya Disemba na Januari, wakati kundi hilo lilipokuwa limetangaza usitishaji mapigano, ikilinganishwa na kipindi sawa na hicho mwaka uliopita.

Hata hivyo, OCHA ilirekodi kuongezeka kwa idadi ya watu wanaolazimika kuhama makwa kwa asilimia 281- hadi watu 5, 000- kati ya kuanza kwa usitishaji mapigano mnamo Novemba 20 na Januari 20, 2013, ikilinganishwa na watu 1, 300 katika kipindi sawa na hicho mwaka uliopita.