Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Radio kuendelea kuwepo leo, kesho na milele: Mbotela

Radio kuendelea kuwepo leo, kesho na milele: Mbotela

Katika ukanda wa Afrika Mashariki, jina Leonard Mambo Mbotela ni maarufu sana kutokana na vile ambavyo mtangazaji huyo mkongwe wa Radio wa nchini Kenya alivyoweza kumudu mikrofoni yake na kuwasiliana na msikilizaji kila uchwao. Miongoni mwa vipindi tulivyofanya katika kuadhimisha siku ya radio duniani ni mahojiano na mtangazaji huyo mkongwe kuhusu mambo mbali mbali ikiwemo hatma ya radio katika zama za maendeleo ya teknolojia ya mawasiliano pamoja na dhima ya radio na uchaguzi wa Kenya. Ninayekukaribisha ni mimi Assumpta Massoi ambapo katika mahojiano yangu na  Bwana Mbotela kwanza kabisa ameanza kwa kuweka msisitizo wa umuhimu wa Radio.