Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Baraza la Usalama lapokea ripoti kuhusu Burundi

Baraza la Usalama lapokea ripoti kuhusu Burundi

Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa, hii leo kwa kauli moja limepitisha azimio nambari 2090 kuhusu Burundi, ambalo, pamoja na mambo mengine, linataja utekelezaji wa mauaji unaodaiwa kufanywa na vyombo vya dola kinyume na sheria, mauaji ambayo yanadaiwa kuambatana na sababu za kisiasa, na limependekeza mahakama ya kimataifa ya uhalifu, ICC kufanya uchunguzi zaidi.

Akizungumza baada ya kura ya azimio hilo, mwakikishi wa kudumu wa Burundi kweney Umoja wa Mataifa amesema kuwa ujumbe wake umesikitishwa na lugha inayotumiwa katika azimio hilo, kwani ripoti ya Katibu Mkuu ambayo imewasilishwa leo inayoonyesha hali kuendelea kuboreka nchini mwake, hasa katika kuimarisha amani na utulivu.