Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

WFP kuanza kutumia bandari ya DSM nchini Tanzania

WFP kuanza kutumia bandari ya DSM nchini Tanzania

Shirika la mpango wa chakula duniani (WFP), limesema kuanzia sasa litaanza kutumia Bandari ya Dar es salaam nchini Tanzania kusafirishia misaada ikiwemo chakula katika nchi za Maziwa makuu pamoja na zile za Pembe ya Afrika.

Hayo yameelezwa na Mkurugenzi wa shirika hilo Bi Ertharin Cousin aliyekamilisha ziara ya siku mbili nchini Tanzania ambapo wakati wa ziara hiyo amekuwa na mazungumzo na viongozi mbali mbali akiwemo Rais Jakaya Kikwete. Kutoka DSM George Njogopa na maelezo zaidi..

(SAUTI GEORGE)