Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Kujumuishwa kwa wanawake katika ajira India kumeshuka: ILO

Kujumuishwa kwa wanawake katika ajira India kumeshuka: ILO

Ripoti mpya ya Shirika la Ajira Duniani, ILO, imesema kuwa idadi ya wanawake ambao hawana ajira, au hawatafuti ajira kusini mwa bara Asia ipo chini zaidi kuliko ile ya wanaume.

ILO imesema, wakati asilimia 80 ya wanaume katika eneo hilo wana ajira au wanatafuta ajira, idadi ya wanawake ipo chini zaidi, ikiwa ni asilimia 32 pekee, huku idadi hiyo ikiwa imeshuka hadi asilimia 29 nchini India. Kwa mujibu wa ILO, idadi hiyo ndogo inatokana na dhana za kitamaduni na mienendo ya kijamii kuhusu wanawake katika mazingira ya kazi, pamoja na ubaguzi.

ILO imesema ili kuongeza nafasi za kazi kwa wanawake, sheria zinazohusiana na ajira zinafaa kuimarishwa katika taaluma zote, pamoja na kupunguza mianya mikubwa ya mishahara na mazingira ya kufanya kazi iliyopo baina ya wanaume na wanawake.