Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Adhaniaye radio inakufa hajui asemalo: Mbotela

Adhaniaye radio inakufa hajui asemalo: Mbotela

Nchini Kenya, akizungumzia siku ya Radio duniani, mmoja wa watangazaji wakongwe nchini humo Lenard Mambo Mbotela amesema adhaniaye radio inakufa hajui asemalo kwani hata sasa wanaotengeneza magari wanalazimika kuweka radio tena za kisasa ili waweze kupata wanunuzi.

Kuhusu nafasi ya radio na siasa amesema kwa sasa Kenya inapojiandaa na uchaguzi mkuu mwezi ujao, radio inatumika kuelimisha umma jinsi ya kutekeleza haki hayo hiyo ya kimsingi kwa amani na utulivu.

(SAUTI YA MBOTELA)

Hata hivyo baadhi ya watangazaji wamesema uwezo wa radio kufikia watu wengi kwa wakati mmoja iwapo hautatumiwa vizuri unaweza kuwa na madhara. Miongoni mwa waliosema hayo ni Vincent Ateya wa kituo cha radio cha Milele FM nchini Kenya.

(SAUTI YA VINCENT)

Kwa vipindi maalum vilivyoandaliwa na idhaa ya kiswahili ya Radio ya Umoja wa Mataifa katika kuadhimisha siku ya Radio duniani hii leo tafadhali tembelea ukurasa wetu www. Unmultimedia.org/radio/Kiswahili