Baraza la Usalama lashutumu jaribio la nyuklia la DPRK

12 Februari 2013

Baraza la usalama la Umoja wa Mataifa limeshutumu vikali kitendo cha Jamhuri ya Kidemokrasia ya watu  wa Korea DPRK kufanya jaribio la nyuklia siku ya Jumanne.

Kauli ya baraza hilo imetolewa muda mfupi baada ya mashauriano ya dharura yaliyofanywa na wajumbe, kufuatia taarifa hizo za jaribio ambapo, taarifa ilisomwa mbele ya waandishi wa habari na Waziri wa Mambo ya Nje na Biashara wa Jamhuri ya Korea Kim Sung-hwan ambayo nchi yake inashikilia urais wa Baraza hilo kwa mwezi Februari.

(SAUTI YA Kim Sung-Hwan)

 

♦ Kupata takwimu za waathirika vitani Ukraine bofya  hapa.
♦ Iwapo ungependa kupokea taarifa kutoka UN News Kiswahili kila wakati zinapochapishwa jisajili  hapa.
♦ Pia unaweza kupakua apu ili kusikiliza matangazo yetu wakati wowote popote ulipo.
♦ Tembelea pia chaneli yetu ya Youtube na pia Soundcloud na Twitter