Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Mkurugenzi Mkuu wa WFP azuru Tanzania

Mkurugenzi Mkuu wa WFP azuru Tanzania

Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Mpango wa Chakula Duniani (WFP), Ertharin Cousin, ameanza ziara ya siku mbili nchini Tanzania hii leo.

Akiwa mjini Dar es Salaam, Bi Cousin anatarajiwa kuzuru eneo la bandari kunakofanyika operesheni za WFP, ili kukagua eneo hilo ambalo ni muhimu kwa kazi ya WFP barani Afrika.

Bi Cousin pia anatarajiwa kukutana na kuzungumzia kazi ya WFP na Rais Jakaya Mrisho Kikwete pamoja na Waziri Mkuu, Mizengo Pinda, pamoja na balozi wa WFP dhidi ya njaa, Howard G Buffett. Hii ndio ziara yake ya kwanza nchini Tanzania kama Mkurugenzi Mkuu wa WFP