Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Uingereza yathibitisha kisa kingine cha homa ya Novel Coronavirus: WHO

Uingereza yathibitisha kisa kingine cha homa ya Novel Coronavirus: WHO

Serikali ya Uingereza imeripoti kuthibitisha kisa cha maambukizi ya homa ya Novel Coronavirus, kufuatia mkazi wake mmoja kuonyesha dalili za maambukizi ya virusi hivyo kuanzia Janauri 26 mwaka huu.

Vipimo vya maabara vimebainisha mgonjwa huyo akiwa na homa ya H1N1 pamoja na Novel Coronavirus, na hivi sasa amewekwa katika kituo cha kutibu wagonjwa maututi. Uchunguzi wa awali umeonyesha kuwa mgonjwa huyo aliwahi kusafiri kwenda nchi za Pakistan na Saudi Arabia.

Idadi ya watu waliothibitishwa kuambukizwa homa ya Novel Coronavirus kufikia sasa ni watu 10, huku watano kati yao wakiwa wamefariki dunia.