Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

IOM yagawa misaada ya dharura kwa wahamiaji raia wa Chad

IOM yagawa misaada ya dharura kwa wahamiaji raia wa Chad

Shirika la kimataifa la uhamiaji IOM limewapelekea chakula , maji na madawa kundi la wahamiaji 32 waliawasili kwenye ofisi za IOM kwenye mji wa Faya Largeau kaskazini mwa Chad juma lililopia baada ya kutimuliwa kutoka nchini Libya.

Makundi matatu ya raia wa Chad wametimuliwa kutoka Libya mwezi Julai mwaka uliopita. Kutimuliwa kwa wahamiaji kunajiri baada ya kurejea nyumbani kwa zaidi ya wahamiaji 150,000 kutoka nchini Libya mwaka 2011 kufuatia kundolewa kwa utawala wa rais Gaddaffi. Jumbe Omar Jumbe ni msemaji wa IOM.

(SAUTI YA JUMBE)