Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Umoja wa Mataifa na Radio za kijamii

Umoja wa Mataifa na Radio za kijamii

Siku ya Radio duniani tarehe 13 mwezi Februari hutoa fursa kwa mashirika ya utangazaji ya kimataifa na kitaifa pamoja na hata radio za kijamii kutathmini jukumu lao adhimu la kuhabarisha, kuelimisha na kuburudisha. Umoja wa Mataifa kupitia mashirika yake umekuwa ukifanya kazi kwa ushirikiano na radio hizo ambazo ziko karibu zaidi na jamii. Hutumia radio hizo kutangaza taarifa mbali mbali ikiwemo usaidizi kwa wakimbizi na hata kutoa mafunzo mbali mbali ya kuboresha jamii.