Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Ban azungumzia uamuzi wa kujiuzulu wa Pope Benedict wa XVI

Ban azungumzia uamuzi wa kujiuzulu wa Pope Benedict wa XVI

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-Moon amezungumzia uamuzi wa kujiuzulu wa Mkuu wa Kanisa Katoliki duniani, Pope Benedict wa XVI tarehe 28 mwezi huu ambapo ametoa shukrani zake kutokana na mchango wa kiongozi huyo katika kuchagiza mashauriano baina ya waumini wa madhehebu mbali mbali duniani.

Taarifa iliyotolewa na msemaji wa Umoja wa Mataifa imemkariri Bwana Ban akikumbuka ziara ya Pope Benedict kwenye makao makuu ya Umoja huo mwezi Aprili mwaka 2008 ambapo aligusia pia changamoto zinazokumba ulimwengu ikiwemo umaskini na njaa na uendelezaji wa haki za binadamu na amani.

Bwana Ban amesema ni matumaini yake kuwa busara alizoonyesha kiongozi huyo wa kanisa katoliki duniani wakati wa uongozi wake, zitabakia mchango muhimu wa kujenga zaidi mashauriano na kuvumiliana.