UNESCO yasaidia uandaaji wa mitaala ya uandishi wa habari Tanzania

11 Februari 2013

Moja ya sababu zinazowatia waandishi wa habari na watangazaji wa Radio hatarini wanapofanya kazi zao ni ukiukaji wa maadili. Waandishi wa habari na watangazaji baadhi yao kwa kukosa stadi sahihi hutangaza habari kupitia radio bila kuzifanyia utafiti au pengine za upande mmoja. Nchini Tanzania ukosefu wa maadili umeripotiwa kusababishwa pia na elimu isiyotosheleza inayotolewa na baadhi ya vyuo vya uandishi wa habari nchini humo. Rose Haji ni Mshauri na Mratibu wa mafunzo kwa Radio Jamii wa Shirika la Umoja wa Mataifa la Elimu, Sayansi na Utamaduni, UNESCO na katika mahojiano yake nami Assumpta Massoi alinieleza kile ambacho UNESCO inafanya kuokoa maisha ya waandishi kwa kuwapatia stadi sahihi za kazi zao. Kwanza anaanza kwa kutaja mambo yanayosababisha waandishi wa habari wawe hatarini nchini Tanzania wanapofanya kazi zao