Mkuu wa UNDP ataka hatua za haraka dhidi ya magonjwa yaso ya kuambukiza

Mkuu wa UNDP ataka hatua za haraka dhidi ya magonjwa yaso ya kuambukiza

Msimamizi wa Shirika la Mpango wa Maendeleo katika Umoja wa Mataifa, Helen Ckark, ametoa wito hatua thabiti na za haraka zichukuliwe ili kusitisha kuenea kwa magonjwa kama vile saratani na kisukari kote duniani, akisema kuwa magonjwa haya yasiyo ya kuambukiza daima yapo kwenye ajenda ya kimataifa maendeleo.

Akizindua msururu wa machapisho katika jarida la masuala ya afya la Uingereza, The Lancet, Bi Clerk amesema kushindwa kuzuia kuenea na ongezeko la magonjwa yaso ya kuambukiza sasa kutachangia gharama kubwa kwa maisha ya mwanadamu na hali yake, na kuwekwa mzigo mkubwa kwa mifumo ya afya, na bajeti za familia na za umma.

Ameongeza kuwa kwa kuweka daima magonjwa hayo kwa ajenda ya kimataifa ya maendeleo, maisha ya watu, nafasi na matumaini yao ya siku zijazo yataboreka, na hivyo kuendeleza maendeleo endelevu kwa ujumla. Ameongeza kuwa mwitikio wa kimataifa dhidi ya HIV na UKIMWI unaonyesha kuwa hatua zikichukuliwa mapema, zinaweza kubadili mkondo wa maradhi.