Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

FAO, IFAD zatiliana saini mpango wa kuwasaidia wakulima wadogowadogo

FAO, IFAD zatiliana saini mpango wa kuwasaidia wakulima wadogowadogo

Mashirika mawili ya Umoja wa Mataifa yametiliana saini ili kufanikisha mpango wa kuwapiga jeki wakulima wadogo wadogo na wale wanaoishi maeneo ya vijijini walioko katika nchi zinazoendelea.

Mashirika hayo lile la chakula na kilimo FAO na lile la maendeleo ya kilimo, IFAD kwa pamoja yamekubaliana kutoa kiasi cha dola za Marekani 875,000 ili kuwaendeleza wakulima wadogo wadogo kumudu gharama za uzalishaji na kuwapa fursa za uwekezaji. Taarifa zaidi na Alice Kariuki

(SAUTI YA ALICE)