Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

CERF yasaidia waathirika wa mafuriko Msumbiji

CERF yasaidia waathirika wa mafuriko Msumbiji

Mfuko mkuu wa misaada ya dharura wa Umoja wa Mataifa CERF, umetoa zaidi ya dola Milioni Tano kwa ajiliya wahanga wa mafuriko nchini Msumbiji.

Mwakilishi mkazi wa Umoja wa Mataifa nchini humo Jennifer Topping amesema licha ya kwamba misaada ya awali ilikwishatolewa lakini bado kuna watu wenye mahitaji makubwa ya kibinadamu nchini Msumbiji.

Amesema msaada huo ni sehemu ya zaidi ya dola Milioni 30 zinazohijika nchini humo kwa ajili ya jumuiya ya kimataifa kusaidia kwa miezi sita watu Laki Moja na Nusu waliokumwba na mafuriko.

Msaada huo wa hivi karibuni utakaoratibiwa na ofisi ya misaada ya dharura ya Umoja wa Mataifa OCHA unawezesha wahanga kupata malazi, chakula, dawa maji safi na salama pamoja na vifaa muhimu.

Kiasi cha watu 105 walipoteza maisha na miundombinu kuharibika kutokana na mafuriko yamwezi Januari nchini Msumbiji.