Kamati ya kutokomeza ubaguzi dhidi ya wanawake yaanza kikao Geneva

11 Februari 2013

Kamati inayohusiana na kutokomeza ubaguzi dhidi ya wanawake imeanza kikao chake cha hamsini na nne leo mjini Geneva, Uswisi kwa kupokea ripoti za vikao vilivyotangulia na kuweka ajenda mpya.

Kamati hiyo pia imemchagua Bi Nicole Amelie kutoka Ufaransa kama mwenyekiti wake mpya, huku wanawake wengine wawili, Violeta Neubauer kutoka mashariki mwa Ulaya na Pramila Patten kutoka Africa wakishaguliwa kama manaibu wake.

Akiongea kwenye kikao hicho, Mkurugenzi wa idara ya mikataba kuhusu haki za binadamu katika afisi ya Kamishna Mkuu wa Haki za Binadamu, Jacob Schneider, ametaja visa vya jaribio la kumuua msichana Malala Yousufzai kutoka Pakistan kwa juhudi zake za kupigia debe elimu ya wasichana na kubakwa na kuuawa kwa msichana wa Kihindi mwenye miaka 23 mwezi Disemba kama mifano ya ukatili dhidi ya wanawake kote duniani, ambao unatakiwa kutokomezwa.