Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

SUDAN na kikundi cha JEM watiliana saini makubaliana ya kusitisha mapigano

SUDAN na kikundi cha JEM watiliana saini makubaliana ya kusitisha mapigano

Serikali ya Sudan na kikundi kikuu cha waasi huko Darfur, cha Justice and Equality Movement, JEM wametiliana saini mkataba wa kusitisha mapigano ambao tayari umeanza kutekelezwa.

Utiaji saini huo uliofanyika Doha, umeshuhudiwa na Kaimu Mwakilishi wa kikundi cha pamoja na Umoja wa Afrika na Umoja wa Mataifa huko Darfur, UNAMID Aichatou Mindaoudou na Naibu Waziri Mkuu wa Qatar, Ahmed Bin Abdullah Al-Mahmoud ambaye nchi yake imekuwa ikiratibu mazungumzo hayo, baada ya makubaliano ya awali ya mwaka 2010 kushindwa kufanya kazi. Taarifa zaidi na George Njogopa.

(SAUTI YA GEORGE)