Chad yaridhia mkataba unaopiga marufuku majaribio ya nyuklia

11 Februari 2013

Idadi ya nchi zilizoridhia mkataba wa kimataifa unaopiga marufuku majaribio ya nyuklia imeongezeka na kufikia 159 baada ya Chad kuridhia mkataba huo.

Katibu Mtendaji wa shirika la kuratibu usimamizi wa mkataba huo Tibor Tóth ameunga mkono hatua hiyo ambayo amesema inaimarisha msimamo wa Afrika wa kutokomeza majaribio ya nyuklia na hatimaye kufikia lengo la kuwa na dunia isiyo na nyuklia.

Chad ilisaini mkataba huo mwaka 1996 na sasa imeridhia tayari kwa kutekeleza.

Barani Afrika, nchi ambazo hazijasaini mkataba huo ni pamoja na Comoros, Jamhuri ya Congo, Misri na Zimbabwe huku nchi zingine duniani ni Marekani, Jamhuri ya kidemokrasia ya Watu wa Korea, Iran na India. Nchi hizo ni lazima zitie saini mkataba huo ili uanze kutumika.

Mkataba huo unapiga marufuku milipuko yoyote ya nyuklia pahala popote au na mtu yeyote na imeweka mifumo ya kufuatilia vitendo hivyo.

 

♦ Kurambaza ukurasa mahsusi wa Siku ya Kiswahili Duniani bofya  hapa.
♦ Iwapo ungependa kupokea taarifa kutoka UN News Kiswahili kila wakati zinapochapishwa jisajili  hapa.
♦ Pia unaweza kupakua apu ili kusikiliza matangazo yetu wakati wowote popote ulipo.
♦ Tembelea pia chaneli yetu ya Youtube na pia Soundcloud na Twitter