Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Mkutano wa vijana kuhusu mazingira wang’oa nanga Nairobi

Mkutano wa vijana kuhusu mazingira wang’oa nanga Nairobi

Mkutano wa  kimataifa wa vijana wa juma moja kuhusu mazingira umeng’oa rasmi hii leo mjini Nairobi nchini Kenya mkutano ambao unawaleta pamoja zaidi ya vijana 800 kutoka pembe zote za dunia.

Kongamano hilo lijukanalo kama TUNZA International Youth Conference on the Environment  linawaleta pamoja vijana kutoka karibu mataifa 100 kujadili hatua ambazo zinaweza kuchukuliwa ili kukabiliana na masuala ya mazingira na vile wanaweza kuwachochea vijana wenzao kuchukua hatua.

Kati ya masuala yatakayojadiliwa kwenye mkutano huo ambao umeandaliwa na shirika la Mazingira la Umoja wa Mataifa UNEP ni pamoja na uhusiano uliopo kati ya afya na mazingira , njia za kuzuia kupotea kwa chakula na wajibu wa mitandao ya mawasilino katika kuboresha maisha. Achim Steiner ni Mkurugenzi Mkuu wa UNEP Achim Steiner.

(SAUTI YA ACHIM)

“Wengi wenu mko kwenye taasisi zikiwemo shule, vyuo vikuu , makampuni au taasisi za serikali kwa hivyo kama unaweza kuchukua masuala haya mawili na kufikiria kuhusu watu wanaokuzunguka wenye unaweza kuchochea ,wale unaoweza kuwaelimisha na kuwafahamisha na kuwafanya kushiriki. Kwa hivyo tunawaona kama mabalozi sio kwa kujadili hali ya dunia tu lakini kwa kuwafanya watu kufanya kitu fulani kwa dunia na hicho ndicho nafikiri mtaenda nacho nyumbani.”